kosa la wengi wetu katika imani - MJUE SANA MUNGU

Breaking

Tafuta ndani

kosa la wengi wetu katika imani




Leo mpendwa msomaji na mfatiliaji wa masomo yetu, aidha kupitia blog au app yetu tuangalie somo la muhimu sana ambalo naamini kwa neema ya Mungu utaweza kujifunza kitu cha ajabu sana , na cha muhimu katika maisha ya imani hata kuufkia uzima wa milele.
je, ni nani ambaye hataki kupata uzima wa milele leo, nani ambaye hataki kuwa rafiki wa Mungu na kumfanya Mungu kuwa Mungu wake?

ni vema kuomba ili somo hili fupi lilete badiliko katika maisha yetu.
Yoh 17:17

omba kwa nafsi yako hapo ulipo ili Roho wa Mungu akusaidie kuelewa kile ambacho ninamaanisha katika somo hili.

KOSA
kosa la wengi wetu ambalo tunalifanya katika imani,
ni jambo ambalo wakati mwingine tumelichukulia kama jambo la kawaida ila ni kosa na hwenda likatufanya kukosa uzima wa milele. nalo ni hili
kutokuwa na imani na Mungu katka Kristo na kuhisi neema yake haitoshi.
ni hivi kuna wakati ambapo tunakosea na hata wakati mwingine makusudi kabisa, na ila nafsi unakuta inatusuta sana kiasi kwamba tunakosa amani, hweda mpendwa umepitia hali hii katika maisha yako.
ila katika hili tunajikuta tunatafuta kwanza tujisikie vizuri ndo twende kwa Mungu!

kuna wengi ambao wanajiona kuwa wadhambi sana kiasi kwamba wanahisi kuwa kwenda kwa Mungu na dhambi zao hawastahili, kwenda katika maombi na makosa yao wanahisi kuwa hawatasikiwa na hivyo huamua kufanya mambo fulani ya kidini kama kusaidia watu, hata wakati mwingie kutoa sadaka na kujisikia vzr na hapo ndo basi wanakuwa na uhuru wa kuomba, ila ujue kuwa ukiwa na dini hii je, tofauti yako na upagani ni ipi?
jiulize hivi mfano wewe ni daktari alafu ukamwona mtu yuko mahututi anakaribia kufa ukamwita njoo nikuhudumuie ila yeye anakujibu kuwa hapana nataka nipone kwanza alafu ndo ntakuja kwako daktari hivi ungemtazamaje mtu huyu?
kadhalika kwetu tunapokuwa na dhambi twataka kujisikia vzr kufanya matendo fulani ya haki ndo alafu twende kwa Mungu hatujui kuwa kufanya hivyo ni sawa a kuunua wema wa Mungu kana kwamba msamaha wa Mungu unanunuliwa ila lah sivyo Mungu anatupenda tulivyo wadhambi
au twasomaje katika maadiko kuwa kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila mtu amwaminiye aspotee bali awe a uzima wa milele Yoh 3:16

basi kumbuka ukiwa unahisi hatia iko moyoni ndo wakati mzuri wa kwenda kwa Mungu na si kusubiri ujisikie vzr na ukifanya hivyo hautokuwa na tofauti na waabudu sanamu kwani wao uzitolea sadaka kwanza ndo baadae hwenda katika kuomba mahitaji yao.
nikuulize swali je, nani alimshauri Yesu kuja kufa kwa ajili yetu?

Yesu alipowasikia, akasema: “Watu wenye afya hawahitaji daktari, lakini wagonjwa wanamhitaji. Mthayo 9:12

pia tujikumbushe fungu moja la  1 Timotheo 1:15
Maneno haya ni yenye kuaminika na yanastahili kukubaliwa kabisa: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni ili kuwaokoa watenda dhambi.+Kati yao, mimi ndiye wa kwanza kabisa.

Yesu alikuja kuokoa wenye dhambi si watakatifu bali wale ambao wako na dhambi hivyo ujionapo kuwa na dhambi ndo wakati safi wa kwenda kwa Mungu usisite hata kidogo mpendwa rafiki nenda bila kusita Yesu anakupeda Moyo wake waumia anapoona kuwa unaona makosa ila bado unatafuta kujistahilisha mbele yake.
kumbuka hakuna hata mmoja kati yetu ambaye yuko na uwezo wa kumshawishi Mungu amkubali hata kidogo yeye hana upendeleo
matendo 10:34
Ndipo Petro akaanza kuzungumza, akasema: “Kwa hakika ninaona kwamba Mungu hana ubaguzi,+ 35  lakini katika kila taifa mtu anayemwogopa na kutenda uadilifu anakubaliwa naye.

pendo la YESU halina ubaguzi, nimeonja upendo wa Yesu kwa kweli hauna kifani yeye ni mwema hata kama unajihisi una dhambi kiasi gani nenda kwake , usiogope hatakufukuza hata kidogo
Yoh 6:37
Wote anaonipa Baba watakuja kwangu, nami sitamfukuza kamwe yeyote anayekuja kwangu.

ubarikiwe sana mpendwa kwa kusoma makala hii kwa ajili yako
install App ya mjue sana Mungu na uwashirikishe wengie ipo play store.
ubarikiwe sana

No comments:

Post a Comment