JITUNZE MGUU WAKO - MJUE SANA MUNGU

Breaking

Tafuta ndani

JITUNZE MGUU WAKO

fungu kiongozi

Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.
mhubiri 5:1
karibu katika somo la leo
Tunapoenda nyumbani kwa Bwana au mahari ba ibada (hekaluni kusali)
ni heri kujikabidhi kwa Mungu na kuwa na kicho kwa Mungu , unajua ndugu kuna wakati watu tunaenda katika ibada kama mazoea tu  ya kawaida na bila kujali , a wakati huo tunajua kuwa kabisa Mungu ni mtakatifu ila tunajisahau sana katika hili kwa baadhi yetu japo sijui wewe msomaji unafanyaje katika hili,

Mungu ni mtakatifu na ni mwema sana na ni mwenye upendo na wakati mwingi tunachukulia upendo wa Mungu kama nafasi ya kufanya mzaha kanisani au sehemu yoyote inayohusisha ibada, tuagalie wana wa israel wao walipojiandaa kukutana na BWANA waliambiwa wajiandae kwa siku tatu , japo sisi hatufanyi hivyo inabidi tukae tumejiandaa muda wote tukimpa heshima Mungu wetu,

hakuna sababu ya kwenda mbele za Mungu kama mazoea tu ya kawaida bila kuangalia unatakiwa kufanya nini, tunapoenda mbele ya watawala wa kifunia mbona tunakuwa na kicho na adabu ila mbele ya Mungu tunajisahau je, twamfanyia Mungu jeuri ?
je, ungekuwa wewe mzazi ungejisikiaje kama kile ambacho unamfanyia Mungu mtoto wako angekufanyia?
mfano mtoto amekuja mbele yako anasema baba au mama nataka tuongee kidogo kua vitu nataka nikueleze.. na unasema sawa unakaa kumsikiliza ila wakati anakaa mara anashika simu anaanza kuchart na hujakaa sawa anaanza kupiga story na marafiki zake waliokaribu naye anasahu kuwa uko naye je ungejisikiaje na ungechukuliaje? je, baada ya story zake anarudi anataka mwendelee mara unapoanza kumsikiliza tena yeye anashika simu tena na kuchart, au anaimba huku kaangalia huko na huko hatulii ungejisikiaje?,
natujiuhoji kweli kama tuna kicho mbele za BWANA mbona twamfayia hiana au twamtia wivu?
basi ni heri kusikia kuliko kutoa kafara ya wapumbavu

tusifanye mambo kwa mazoea hivi mfano akikasirika siku moja kwa ajli ya ujinga wetu itakuwaje?
na tuwe na kicho mbele za BWANA  uendapo katika ibada yoyote, iwe yumbani au kanisani basi tunza akili yako weka mipaka, epuka story na watu wengine huwapo katika ibada ni vyema mpe Mungu heshima yake.
na hata wakati wa mazoezi ya kwaya ni vema napo kukawa na kicho cha Mungu tusimkwaze Rho kwa mizaha , na mambo yasiyopasa .malaika hawapendi kupeleka taarifa mbaya kuhusu sisi na kicho kiwepo.
isaya 1:16,
Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;

pia tuwakumbuka wana wa Haruni ambao walikwenda hovyo mbele za BWANA na moto ukatoka ukawateketeza .
Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana, ambao yeye hakuwaagiza. 
Kisha moto ukatoka hapo mbele za Bwana, nao ukawala, nao wakafa mbele za Bwana. 
Ndipo Musa akamwambia Haruni, Jambo hili ni hilo Bwana alilolinena, akisema, Nitatakaswa mimi katika hao wanikaribiao, nami nitatukuzwa mbele ya watu hao wote. Haruni akanyamaza kimya.   walawi 10:1-3
 tuangele namna tunavoenenda
 tuombe Mungu atusaidie na kutukumbusha maana tunatabia ya kusahau na atutie nguvu maana bila yeye hatuwezi chochote.

kumbuka kuwajulisha wapendwa wa install app ya mjue sana Mungu kujifunza zaidi iko play store search mjue sana Mungu utaipata

No comments:

Post a Comment