1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.1 Yoh 3:1
Kuna wakati katika maisha haya kabla hayajafikia kikomo huna budi kukaa Na kutafakari wewe ni nani?
Na unaishi kwa ajili ya nini Na je faida yako ni IPI.
Tujue kuwa Mungu ametupenda hata kuona vema kutupatia nafasi ya kuwa watoto wake, ila jambo LA ajabu wengi twaishi kama watumwa Na wengi wetu tumezibwa macho Na adui wa haki ambaye ni ibilisi tusifahamu kuwa sisi twatakiwa kuwa wana wa Mungu .
Alitoa zawadi ya pekee kuliko zote si kwa faida yake Bali faida yetu ya sisi kuurithi uzima wa milele kupitia kumwamini Yesu Kristo.
Amini sasa kuwa unaweza kuwa mwana wa Mungu. Na kupata haki zote azistahilizo mtoto,ulinzi,chakula faraja ,malazi,nk. Zaidi uzima wa milele kwanini kumg'ang'ania shwtani hakuna kitu chema ambacho atakuoatia ,yeye ni adui wa haki ya Mungu Na kamwe hataki ujue namna gani Baba yako anavyokupenda anakudanganya Na raha za kitambo akitafuta nafasi ya kukuua.
Amua sasa kummwamini Mungu ,mwamini Yesu Kristo nawe utapata raha nafsini mwako.
Amua sasa kummwamini Mungu ,mwamini Yesu Kristo nawe utapata raha nafsini mwako.
No comments:
Post a Comment