
Fungi kiongozi,
Zaburi 17:8
Unilinde kama mboni ya jicho unifiche chini ya uvuli was mbawa zako.
Kuna wakati ambapo umeona kuwa unapitia katika kipindi kigumu? Na he kunawakati ambapo unaona kuwa kana kwamba wewe peke yako ndo uneibeba dunia yote?
Na basi sisi kama wanadamu tunapitia wakati mwingi wa machozi , ila tumepata nafasi ya kuomba,
Na tumwambie Mungu awe kings yetu.
Ombi hili la mtumishi wa Mungu ni la kwetu pia , kuongea na Mungu kama rafiki,
Unajua kuna mambo Fulani tunayaogopa ila hatukupaswa kuogopa .
Katika biblia imeandikwa mahali Fulani kuwa wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, sasa jisikie kuwa mtoto wa Mungu na hivyo kama una mzazi anayekupenda utaenda mbele zake na kuegama kifuani kwake kama kueleza utaeleza yote yaliyo moyoni mwako, kwani in baba,
Tuangalie mfano wa watoto wadogo ambao wanakuwa wameegama kifuani mwa wazazi wao mwa baba zao, wanatulia tuli! Kana kwamba dunia yote no ya kwako.
Nikuulize kitu mpendwa tu tena kitu rahisi
Mara ya mwisho kutulia kifuani mwa Mungu ni lini? Au hujui kuwa unapendwa ? Laiti ungelijua kuwa Mungu anakupenda kyliko kitu chochote, wanadamu tunapendana ila tunaachana kwa vitu vidogo sana ila kwa Mungu upendo wake kwetu unazidi mauti.
Turejee kwake na masumbufu yote tumweleze yote pasi kuficha chochote.
Nina kawaida moja na imekuwa baraka katika maisha yangu ,napohuzunila au kufurahi sifichi kwa Mungu namwambia yote ,yeye najua anajua ila nafurahi kuongea nae,na mengi hunipatia Tumaini kuwa anayashughulikia nami natulia .
Bwana ni mwema siku zote.
Pendo la Yesu kwetu halina kifani yeye ni ngao yetu.
Mungu na awe maji yako ukiwa na kiu.
Na awe chakula chako unapokuwa na njaa na awe kivuli chako juani.
Yesu anakupenda,
Washirikishe wengine ,kuinstall app ya mjue sana Mungu iliyopo play store.
Ubarikiwe
No comments:
Post a Comment