
hata jibu moja la makosa tu lingeharibu nafasi yako ya kufaulu na hivyo ungekuwa sawasawa na mtu ambaye kakosa kila swali.
kwa maaa fulani ndivyo ilivyo na wokovu wetu tunahitaji kupata alama zote kamili ili kupata wokovu, utakatifu kamili, utii kamili wa sheria ya Mungu.
Mtu mtakatifu kuliko wote ambaye ana dosari ndogo sana katika tabia, yuko sawasawa na mbadhilifu, fisadi na mpotovu zaidi. Bila kuwa na haki kamilifu sisi tumepotea.
turudi katika kisa chetu ambacho tumeanza nacho hapo juu kama unakumbuka kuwa sasa umeshindwa kupata alama zote katika mtihani na kila somo , na mmoja (mwanafunzi) ambaye si tu kuwa kapata alama zote lakini akajitolea kukushirikisha alama zake, yaani alama zake zinakuwa zako.
ambayo ndiyo njia pekee kwa hiyo ungeweza kufaulu.
Yesu pekee aliye haki kamilifu na habari njema ya njili ni kuwa anatoa haki hiyo kamilifu kwa wale wote ambao wanadai haki hiyo kwelikweli kwa imani.
sio mwelekeo wa Ibrahimu kwa wema na utakatifu wala urithi wake ulifaa kuangaliwa ,lakini Ibrahimu alikuwa wa pekee kama ambavyo yeyote kati yetu anaweza kuwa wa pekee.
Ibrahimu aliamini kuwa Mungu anaweza kumbadilisha , angeweza kufanya kazi kupitia kwake, alimwamini Mungu Mungu akamkubali kama mwenye haki na Mungu akamfanya aweze kutenda haki.
kumbuka kuistall app ya Mjue sana Mungu ambayo ipo playstore. click neno Mjue sana Mungu
No comments:
Post a Comment