Adamu na hawa walikuwa wamesimama kando ya maiti ya mtoto wao wakilia / muda mfupi kabla ya hapo , alikuwa amejaa furaha na uzima.
Sasa alikuwa amekuwa mhanga wa muuaji/ kwasababu ya hasira kali na wivu, ndugu yake mwenyewe aliinua silaha iliyoleta msiba katikafamilia ya kwanza kabsa hapo dunianiHawa angeweza kuuliza swali lile ambalo kina mama wengi wamekuwa wakiuliza "kwanini Mungu? Kwanini jambo hili limtokee mtu mwema kiasi hiki asiye na hatia? Lakini Hawa angeweza kuelezea vizuri zaidi sababu ya janga kama hilo kuliko mama mwingine yeyote, kwani wimbi la matatizo, ugonjwa na kifo lilitokana na uasi wake
sitaisahau siku ambayo mama yangu alikufa. nilipofika nyumbani, mwili wake ulikuwa umeshapelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
kila mmoja kati ya sisi watoto alikuw ameshtuka. kisha nikaenda kumtafuta baba yangu nilimkuta chumba cha chini akiwa analia na kuuliza" Kama Mungu ni mwema hivyo, anawezaje kumchukua mama anayehitajiwa sana na watoto wake saba?"
swali hilo lilidumu kichwani mwangu kwa miezi kadhaa nikiwa natafuta jibu. nilipata jibu katika Biblia, na ningependa kukueleza juu ya jibu hilo katika somo hili.
1. Dhambi ilianzia wapi?
"Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo." 1yoh 3:8 "Yule.... nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na shetani" Ufu 12:9
shetani aitwaye pia Ibilisi ndiye mwanzilishi wa dhambi, bila ya maandiko, chanzo cha uovu kisingejulikana.
2. Shetani alikuwa akiitwa nani kabla ya kuasi? Alikuwa akishi wapi?
" Jinsi ulibvyoanguka kutoka mbinguni, ewe Nyota ya alfajiri , mwana wa asubuhi" isa 14:12
" Akawaambia, nillimwona shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme" Luka 10:18
" Ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu " Ezekiel 28:14
Shetani alikuwa akiishi mbinguni ali[oasi. Jina lake aliitwa Lusifa yaani , "Yota ya alfajiri"
3. Lusifa alitoka wapi? Alikuwa na cheo gani? Biblia inamwelezeaje?
"wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye" eze 28:14.
"wewe wakitia muhuri kipio, umejaa hekima , na ukamilifu wa uzuri...... kila jiwe la thami lilikuwa kifuniko chako..... kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako, katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.... ulikuwa mkamilifu katikanjia zako hata uovu ulipoonekana ndani yako" Eze 28:12-15
Lusifa alikuwa malaika aliyeumbwa na Mungu. Alikuwa mkamilifu katika hekina na uzuri na alisismama karibu na kiti cha enzi cha Mungu.
4.Ni jambo gani lilitokea katika maisha ya lusifa lililomfanya aasi? Kisha alifanya dhambi gani ya kukufuru?
"Moyo wako uliinuka kwasababu ya uzuri wako umeiharibu hekima yako kwasababu ya mwangaza wako" Eze 28:17
"Nawe ulisema moyoni mwako ..... nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu, Nami.... nitafanana na yeye Aliye juu"
isaya 14:13-14.
kiburi, wivu kutokuridhika na kujiinua nafsi viliinuka katika maisha yake. Lusifa aliamua kumwondao Mungu katika kiti chake cha enzi na kudai kuwa yeye ndiye aabudiwe. ulikuwa ni uhaini wa hali ya juu kabisa.
5.Kulitokea nini mbinguni baada ya Lusifa kuasi?
"Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. " ufu 12:7-9
kutoridhika kwa Lusifa kulizaa uasi wa wazi dhidi ya Mungu. theluthi ya malaika wa mbinguni waliungana naye katika jaribio la kumpindua Mungu. Matokeo yake Lusifa na wafuasi wake walitupwa kutoka mbinguni
6.Makao makuu ya shetani kwasasa yako wapi? Ana hisia gani juu ya wanadamu?
"Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo". Ayub 2:2
"Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu. " Ufu 12:12
mshitaki wenu ibilisi kama siba aungurumaye , huzungukazunguka , akitafuta mtu ammeze.
makao makuu ya shetani ni duniani na siyo jehunum kama wengi wanavyofikiria. anawachukua wanadamu na lengo lake ni kumwumiza Mungu kwa kukuangamiza wewe.
7.Mungu aliwazuia Adamu na Hawa kufanya jambo gani? Adhabu yao ilikuwa ni nini kama wasingetii?
"walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika." mwa.2:17.
Adamu na Hawa hawakupaswa kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya na adhabu yake ilikuwa ni kifo kama wangeasi
8.Je,Kula kipande cha tunda lilikuwa jambo baya kiasi hicho? kwanini Adamu na Hawa waliondolewa katika Bustani ya edeni?
"Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi" yak 4:17
"Dhambi ni uasi" 1yoh 3:4.
"Atendaye dhambi ni wa ibilisi" 1 yoh 3:8
"2 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima." Mwa 3:22,24.
kula tunda walilokatazwa kuliwafanya Adamu na Hawa kuwa washiria wa shetani, ambaye ni adui mkuu wa Mungu.
9.Je, Biblia hufunua mambo gani ya ajabu juu ya mbinu za shetani katika kuumiza kudanganya , kukatisha tamaa na kuangamiza watu wa Mungu?
BIBLIA INASEMA
Hudanganya /hutesa ufu 12:9,13
husiingizia/huua ufu 12:10; Yn 8:44
hufanya vita na watu wa Mungu ufu 12:17
hutia gerezani ufu 2:10
hufanya miujiza/uongo ufu 16:13,14; Yn 8:44
huleta magonjwa/maumivu Ayu 2:7
Ni mzushi"ibilisi" maana yake ni mzushi
hunukuu/hupotosha Biblia Mat 4:5,6
hutega/huvizia 2 Tim 2:26; Pet 5:8
hufunga /huchochea usaliti Lk 13:16;Yn 13:2,21
huwaingia watu/huzuia Lk 22:3-5; 1 The 2:18
hujifanya malaika wa nuru 2 Kor 11:13-15
mapepo wake hujifanya wachungaji 2 Kor 11:13-15
huita moto kutoka mbinguni Ufu 13:13
10.Je, majaribu na mikakati ya shetani inauwezo na mafanikio kiasi gani?
Aliwashawishi theluthi ya malaika(ufu 12:3-9)
Adamu na Hawa (Mwa 3) watu wote kasoro wanane kwenye siku za nuhu( 1 pet 3:20) Atawafanya waliopotea wajisikie wako salama (Mt 7:21-23)
karibu dunia nzima itamfuata (ufu 13:8) ni wachache watakaookolewa (Mt 7:14; 22:14)
Nguvu ya udanganyifu wa shetani katika siku za mwisho itakuwa kubwa kiasi kwamba karibu dunia nzima itamfuata.
11.Je,Ibilisi atapata lini na wapi adhabu yake? Adhabu yake itakuwa ni nini?
"Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.
Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno." Math 13:40-42.
"Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele " Ufu 20:10
"Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake" Math 25:41
"Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.
19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele". Eze 28:18,19
Mwisho wa dunia shetani atatupwa katika ziwa la motoambao utamfanya kuwa majivu na kukomesha kuwepo kwake milele
12.Ni jambo gani litakalomaliza dhambi? Je, dhambi itainuka tena?
"Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu."
(soma pia Flp 2:10,11; isaya 45:23)
mateso hayatainuka mara ya pili nah 1:9
mambo mawili muhimu yatamaliza tatizo la dhambi. kwanza viumbe vyote , mbinguni na duniani pamoja na ibilisi na malaika zake kwa hiari yao wenyewe watapiga magoti na kukiri hadharani kuwa Mungu ni mkweli asiye na upendeleo , na mwenye haki. hakuna swali litakalobaki bila kujibiwa. Waovu wote watakiri wazi kuwa wamepotea kwasababu waliukataa kwa ukaidi upendo na wokovu wa Mungu.watakiri kwamba ili haki itendeke ni lazima wafe. Wote watakiri kwamba wanastahili mauti ya milele.
Pili, dhambi itaondolewa ulimwenguni kwa kuteketezwa kabisa kwa dhabi, wenye dhambi, Ibilisi na malaika zake. Mungu yuko thabiti katika jambo hili: Dhambi haitainuka tena kuuchafua ulimwengu wa Mungu.
13.Ni nani anayefanya kuondolewa kabisa kwa dhambi ulimwenguni kuwa jambo la uhakika?
"Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. " 1 Yoh 3:8
"Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,"
Ebr 2:14
Kwa njia ya maisha yake, kifo chake na kufufuka kwake, Yesu alifanya kuondolewa kwa dhambi liwe jambo la uhakika.
14.Je,Mungu Baba ana hisia gani juu ya watu?
"kwa maana Baba mwenyewe awapenda" Yn 16:17 (soma pia Yn 3:16; 17:22,23)
Baba awapenda watu kama vile Mwana awapendavyo, kusudi kubwa la Yesu lilikuwa kudhihirisha tabia ya Baba yake katika maisha yake ili watu wajue jinsi alivyi na upendo, mchangamfu na mwenye kujali,
" Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. " Yn 5:19
Shetani amezua uongo mwingi kuhusu tabia ya Bba kwamba hajali ni mwenye sheria kali mkalina asiyeingilika(ambazo ni tabia zake mwenyewe) Hata matendo yake mabaya katika majanga huyaita "kazi ya Mungu" Yesu alikuja kufuta uzushi huu na kuonesha kuwa Baba yetu wa Mbinguni anatupenda zaidi ya mama apendavyo mtoto wake.
"Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe"
isaya 49:15
somo kuu la Yesu ilikuwa uvumilivu wa Mungu, upole na rehema tele.
Baba anasubiri kwa hamu ili kuwafanya watu wawe na furaha kuuBba yetu wa Mbinguni amewaandalia makao mazuri ajabu ndoto zetu haziwezi kulingana na yale yanayotungoje! anasubiri kwa hamu kuwakaribisha watu wake siku ile furaha ya kurejea nyumbani ambayo i karibu sana . Tunapaswa kuitangaza mbiu hii, N atuwe tayari. tuko katika siku za mwisho.
Baba anakupenda kama vile Yesu anavyokupenda Je, unadhani kuwa hii ni Hbari njema?
Kma hii ni habari njema kwako, je utamruhusu sasa Mungu atimize mapenzi yake katikamaisha yako, kwa kujifunza na kuyafanya mapenzi yake kama yalivyo katika Biblia?
UAMUZI WANGU NI............................................
Kama unaswali au ombi au chochote Karibu sana
ReplyDelete